For a better experience please change your browser to CHROME, FIREFOX, OPERA or Internet Explorer.
KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI

KILIMO BORA CHA VITUNGUU MAJI

Utangulizi
Vitunguu maji kwa kitaalamu hujulikana kama Allium cepa kwa kiingereza huitwa Bulb Onions.Vitunguu ni zao muhimu sana sio kwa matumizi ya ndani tu lakini pia ni zao la kibiashara linaloweza kukuletea kipato kikubwa. Vitunguu ni zao la bustani ambalo lipo kwenye kundi la mboga (vegetables). Zao hili ni maarufu kutokana na thamani ya virutubisho ilivyonavyo na ladha yake kwenye mapishi ya vyakula mbalimbali.


ASILI YA VITUNGUU

Vitunguu vinaaminika, vilianzia Uturuki (Turkey) japo maandiko mengine yanajumuisha pia, Iran, Afghanistan, Pakistan na Kaskazini mwa China kama ndio asili ya vitunguu maji.


Uzalishaji wa Vitungu Duniani
China ndiyo inaongoza kwa uzalishaji wa vitunguu vingi duniani, ikifuatiwa na India kasha Marekani. Kwa Afrika Nchi zinaoongoza kwa uzalishaji wa Vitunguu ni Misri, Algeria, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini na Niger. Kwa Africa Mashariki Tanzania ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Kenya. Kwa uzalishaji wenye tija Korea ndiyo inayoongoza, ikifuatiwa na marekani kisha Uhispania (Spain). Katika uzalishaji wenye tija kubwa (high productivity) tunamaanisha wingi wa mavuno kwa eneo (ekari au hekta). Korea wao wanavuna Tani 26.8 kwa ekari (sawa na Tani 67 kwa hekta) kwa vipimo vya magunia ni sawa na magunia 223 kwa ekari moja. Marekani wanavuna tani 22.8 kwa ekari (sawa na tani 57 kwa hekta), kwa vipimo vya magunia ni sawa na magunia 190 kwa ekari. Uhispania wao wanavuna magunia 180 kwa ekari. Kwa Tanzania wakulima wengi hupata gunia 80-120 kwa ekari. Wachache sana wanaozingatia kanuni bora za kilimo vizuri hupata gunia 120-150 kwa ekari.


Uzalishaji wa Vitunguu kwa Tanzania
Kwa Tanzania vitunguu huzalishwa katik maeneo na hali ya hewa mbalimbali, lakini kwa wingi
vitunguu huzalishwa Arusha (Karatu โ€“ Mangโ€™ola), Singida, Morogoro na Dodoma (Chikopelo,Dabalo na Mpwapwa-lumuma), Ruaha mbuyuni Iringa, Gange -kilimanjaro na nk.


Hapa nchini vitunguu hulimwa kipindi chote cha mwaka kutegemeana na eneo, lakini uzalishaji mkubwa au msimu mkubwa wa vitunguu huonekana kati ya mwezi June na September (mwezi wa 6 hadi wa 9),

Hivyo mara nyingi miezi hiyo Vitunguu hua na bei ndogo maana uzalishaji ni mkubwa. Msimu mdogo (low season) wa Vitunguu kwa Tanzania ni kati ya Mwezi wa Kwanza hadi wa Nne (January hadi April). Kipindi hichi maeneo mengi hua na Mvua nyingi ambayo kwa kwawaida huathiri kilimo cha Vitunguu, hii hupelekea wazalishaji wachache kumudu kuzalisha vitunguu. Hii pia huchangiwa na gharama kubwa za uzalishaji kipindi cha mvua, na mavuno yake hua kidogo kulinganisha na msimu wa kiangazi. Kipindi hiki mara nyingi bei ya Vitunguu hua juu zaidi.


AINA ZA MBEGU ZA VITUNGUU
Kuna aina tatu za mbegu za vitunguu.


Aina ya Kwanza: Mbegu za Kienyeji:
Hizi ni zile mbegu zinazozalishwa na wakulima wenyewe. Mara nyingi mbegu hizi zinakua hazijathibitishwa na wataalamu kutoka taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu (TOSCI). Wakulima wanazalisha mbegu hizi na kuwauzia wakulima wengine kwa kutumia kipimo cha kilo au debe. Wakulima wengi hupendelea mbegu hizi za kienyeji kwa vile bei yake ni ndogo. Mbegu hizi maeneo mengi huuzwa kati ya 20,000 hadi 30,000 kwa Kilo moja ya mebgu. Kutokana na kwamba mbegu hizi zina ubora mdogo, mkulima inambidi atumie mbegu nyingi ili kutosheleza mahitaji ya ekari moja. Kwa ekari moja mkulima hutumia kilo 6 hadi 10 za mbegu hizi ili kutosheleza. Kama mtaalamu wa kilimo simshauri mkulima anayetaka kulima kibiashara kutumia mbegu hizi za kienyeji kwa maana hata Mavuno yake hayatabiriki. Ila Sio kwamba mbegu zote zinazozalishwa na wakulima ni mbaya, hapana.
Upo utaratibu wa wakulima kuzalisha mbegu kitaalamu kwa kufuata utaratibu ulipo kisheria. Mbegu hizo zinazozalishwa na wakulima kitaalamu huitwa mbegu za daraja la kuazimiwa (quality declared seeds) au kwa kifupi huitwa QDS. Mbegu hizi za QDS zina mipaka yake ya eneo la kutumika. Na wazalishaji wa QDS lazima wapate mafunzo na wasajiliwe na Taasisi ya Uthibiti Ubora wa Mbegu (Tanzania Official Seed Certification Institute) au kwa kifupi TOSCI. TOSCI pia wana utaratibu wa kufanya ukaguzi na kutoa kibali cha mbegu hizo za QDS kuuzwa kama zimekizi vigezo husika. Kama hazijakizi mbegu hizo haziruhusiwi kuuzwa kwa wakulima.
Aina ya Pili: Mbegu za Kawaida zilizizoboreshwa (Open Pollinated Varieties) au kwa kifupi huitwa OPV. Mbegu hizi zimezalishwa kitaalamu kwa njia ya Uchavushaji ya wazi (Open Pollination). Mbegu hizi ndio zinazouzwa kwa wingi na makampuni ya mbegu. Bei yake ni kati ya 60,000 hadi120,000 kwa kilo. Hii inategemeana na kampuni na aina ya mbegu. Mbegu hizi kwa ekari moja utatumia Kilo 3 hadi 4. Mfano wa mbegu za OPV ni: Bombay Red, Red Creole, Tajirika, Meru Super n.k.
Aina ya Tatu : Mbegu Chotara (Hybrid):
Hizi ni aina ya mbegu zinazozalishwa kitaalamu sana kuliko hizo aina nyingine nilizozitaja hapo juu. Mbegu hizi hua na sifa za kipekee, kama vile kua na mavuno mengi, kuwa na ukinzani kwa baadhi ya magonjwa, kukomaa haraka n.k. Nyingine hutengenezwa kutokana na sifa maalumu zinazohitajika na walaji au soko, kama vile rangi, ukubwa (size), harufu, ladha n.k. Pia mbegu hizi huuzwa ghali zaidi. Bei yake ni kati ya 300,000 hadi 600,000 kwa Kilo moja. Kilo moja na nusu au Kilo 2 hutosha kwa ekari moja. Mfano wa mbegu hizi ni kama Neptune F1, RedStar F1, JAMBAR F1 n.k
Mahitaji ya Kiikolojia kwa ajili ya uzalishaji wa Vitunguu (Ecological requirements)


Hali ya Hewa:
Vitunguu hustawi maeneo ambayo hayana mvua nyingi, yenye baridi kiasi.
Udongo :
Vitunguu hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha. Udongo ambao ni mlaini usioshikamana (loose soil) wenye kuruhusu mizizi kupenya kirahisi, unaohifadhi unyevunyevu kama mfinyanzi tifutifu. Udongo unaotuamisha maji haufai. Tindikali (Soil pH) ya 5.5-6.8
Maandalizi ya shamba la Vitunguu:
Lima shamba lako vizuri, angalau utifue/ufukue udongo kwa kina cha sentimita 15 kwenda chini. Shamba lako lilimwe wiki 2 au 3 kabla ya upandaji wa vitunguu. Lainisha udongo au kwa kitaalamu inaitwa Harrowing. Yaani yale mabonge makubwa makubwa ya udongo yanagongwa na kutengneza udongo mlaini. Harrow ifanyike wiki 2 au 3 baada ya kulima. Zipo trekta zinazofungwa mashine ya kufanya harrowing. Tengeneza matuta au vitalu kwa ajili ya kupandia. Kwa matokeo mazuri matuta ya vitunguu yawe yale ya kuinuka (raised bed) angalu mwinuko wenye urefu wa sentimita 20-30. Upana wa tuta uwe mita moja au mita moja na nusu na urefu usizidi mita 6.


Upandaji wa Vitunguu:
Vitunguu vinaweza kupandwa kwa njia mbili:
Njia ya kwanza: Upandaji wa moja kwa moja (direct planting). Namna ya Kupanda vitunguu kwa njia ya moja kwa moja: Andaa shamba vizuri, udongo uwe mlaini, usiwe na mabongemabonge ya udongo. Weka mbolea ya samadi kwa kutawanya (broadcasting) kisha ichanganye vizuri na udongo. Mbolea ya samadi inayotosha kwa ekari moja ni tani 16 au pima udongo kupata kiwango sahihi zaidi. Baada ya kuchanganya vizuri samadi kwenye udongo, tengeneza mistari (drills) yenye kina cha sentimita 2.5 na yenye umbali wa sentimita 10cm kutoka mstari hadi mstari. Kumbuka hii mistari ni kama mifereji midogo mwembamba ambayo itatumika kuweka mbegu. Hivyo zingatia vipimo. Weka mbolea ya kupandia kwenye hiyo mistari uliyotengeneza. Mbolea hii inapaswa kua na kirutubisho cha Phosphorous (Phosphate fertilizer). Mfano wa mbolea za kupandia ni kama DAP, MAP, TSP n.k. Ukishanyunyizia mbolea ya kupandia ichanganye vizuri na udongo. Sia mbegu kwenye hiyo mifereji halafu funika kwa udongo. Kisha mwagilia mara kwa mara kadri mahitaji yanavyoongezeka. Hapa ina maana kwamba kadri mmea unavyokua ndivyo unahitaji maji mengi zaidi. Mimea ikashakua, punguza mimea, na uache sentimita 5 (cm) kati ya mmea na mmea. Ile mimea unayoipunguza kwa kuingโ€™oa inaweza kupandwa sehemu nyingine. Hivyo basi nafasi ya mimea itakua ni 10 cm X 5 cm. Yaani mstari hadi mstari ni sentimita 10 na nafasi ya mche hadi mche ni sentimita 5.


Njia ya pili: Upandikizaji wa miche (transplanting).
Hapa Miche inakuzwa kwenye kitalu kwa wiki 6 hadi 8 tangu kisia mbegu kisha inahamishiwa shambani. Inakadiriwa kwamba wiki 6 hadi 8 miche itakua imefikia kiwango kizuri cha ukuaji kwa ajili ya kuhamishiwa kwenye shamba kuu (main field). Hii ndio njia inayoshauriwa zaidi na ndiyo inayotumia na wakulima wengi wa vitunguu.


Jinsi ya Kukuza Miche Vitunguu kwenye Kitalu
Tengeneza matuta yaliyoinuka (raised seed beds) yenye upana wa mita 1 na urefu utakaopenda. Urefu mzuri wa tuta unaweza kuanzia mita 2 hadi 6. Idadi ya matututa itategemea na wingi wa mbegu unazotaka kusia. Weka Mbolea ya samadi iliyooza vizuri. Itawanye vizuri kwenye matuta ya kitalu. Weka Mbolea ya kupandia ya viwandani kama TSP au MAP au DAP. Kisha changanya vizuri na udongo. Hakikisha Samadi, mbolea ya ya Kupandia TSP/DAP vyote vinachanganyika vizuri kwenye udongo. Tengeneza mistari ambayo iko kama mifereji midogo yenye urefu wa sentimita 2. Mistari hiyo iwe umbali wa sentimita 5 kutoka mstari hadi mstari. Sia mbegu za vitunguu kwenye mistari hiyo kisha funika na udongo kidogo. Funika tuta lako kwa nyasi zilizokauka. Nyasi zinasaidia kutunza unyevunyevu wa udongo pamoja na joto la udongo litakalosaidia miche kuota vizuri.
Mwagilia maji mara kwa mara. Umwagiliaji unapaswa kuzingatia unyevunyevu wa udongo. Epuka kuzidisha maji kwenye kitalu maana husababisha magonjwa ya fungus (fungal diseases)kama Kinyausi (Damping Off).Ondoa Nyasi mara mimea inapoanza kuchomoza juu ya udongo.

Kama ni msimu wa jua kali, tengeneza kichanja ambacho juu yake utafunika na nyasi chache ili kupunguza ukali wa mionzi ya jua kwenye miche. Kila tuta unaweza kulijengea kichanja chake. Ngโ€™oa magugu kwenye kitalu au pulizia viuagugu. Hakikisha kitalu hakina magugu wakati wote, kwa maana vitunguu vina mizizi mifupi (shallow roots) na haiwezi kushindana na magugu. Pandikiza miche yako kwenye shamba kuu mara miche inapofikia urefu wa sentimita 15. Mara nyingi huchukua muda wa wiki 6 hadi 8 toka kusia mbegu hadi kufikia kupandikizwa. Maeneo ya joto ukuaji wa miche ni wa haraka zaidi, chini ya wiki 6 miche inakua tayari.


Upandikizaji wa Vitunguu
Vitunguu vinapsawa kupandikizwa wakati wa asubuhi au au jioni. Wakati wa jioni ndio mzuri zaidi wa kuhapandikiza miche. Miche inapaswa kupandwa kina kilekile kama ilivyokua kwenye kitalu. Yaani mche unapongโ€™olewa kwenye kitalu kuna sehemu ilikua chini ya ardhi. Kwenye kupandikiza urefu uleule uliokua chini ya ardhi wakati mche ulipokua kwenye kitalu ndio unapaswa kufunikwa na udongo wakati wa kupandikiza. Nafasi ya upandaji wa miche unapaswa kua sentimita 10 kwa 5-8 (10 X 5-8 cm). Yaani urefu wa mstari na mstari uwe sentimita 10 na nafasi ya mche na mche iwe sentimita 5 – 8. Nafasi inaweza kutoafutiana kidogo kulingana na aina ya mbegu, lakini pia kulingana na ukubwa wa kitunguu unachotaka. Ukitaka vitunguu vikubwa, nafasi inaongezeka, yaani vinapandwa mbalimbali. Ukitaka vitunguu vidogo unapunguza nafasi, yaani unapanda karibukaribu.


NB .
Kwa leo naomba tuishie hapa, tutaendelea kesho muda kama wa leo. Mada ambazo bado ni;
1) Mbolea -atafundisha mtaalamu wa mbolea kutoka Yara.
2) Visumbufu vya vitunguu (Magonjwa, wadudu na magugu)
3) Uvunaji wa vitunguu
4) Uhifadhi wa vitunguu.
Ahsanteni na karibuni kwa maswali yanayohusu somo la leo tu mpaka tulipofikia.
Palizi kwenye zao la vitunguu
Mmea wa kitunguu una mizizi mifupi, hii husababisha kutunguu kuathirika sana na ushindani na magugu. Mizizi mifupi ina maana huufanya kukosa uwezo wa kustahimili ushindani wa magugu. Magugu yana uwezo mkubwa wa kufyonza virutubisho ardhini kuliko kitunguu, na ndio maana magugu hukua kwa haraka kuliko mazao. Hivyo inashauriwa katika shamba la vitunguu l hakikisha unafanya palizi kwa wakati. Idadi ya palizi inategemea na aina na wingi wa magugu wa eneo husika. Kwenye maeneo yenye magugu mengi, palizi hufika hadi 4, na kwa maeneo ambapo magugu sio tatizo palizi mbili zinatosha. Kuna mbinu mbalimbali za kfuanya palizi kama matumizi ya viuagugu za kudhibiti magugu (herbicides), palizi ya mkono (hand weeding) na uwekaji wa matandazo (mulching).
Viuagugu ambavyo vinafanya vizuri.
A) Viuagugu vinavyopulizwa kabla ya magugu kuota baada ya kupandikiza vitunguu.
โžข Volmet 960 EC (metolachlore 960 g/l)-Kiuagugu hiki kinazuia magugu kwenye shamba vitunguu yasiote.
Inatumikaje ?
Baada ya kupandikiza vitunguu unapima kiuagugu hiki kiasi cha 120 -150 ml kwa bomba lita 20 kisha unapulizia kwenye udongo baada ya kupanda vitunguu, wakati wa kupulizia ni lazima udongo uwe na unyevu wa kutosha. Haina madhara kabisha kwenye vitunguu. Pulizia kabla ya magugu kuanza kuota mara tu baada ya kuotesha,isipite siku 7 maana magugu yataanza kuota.
โžข Volmethalin 500 EC_ (pendimethaline 500 g/l), Fist Super 456 C_ (Pendimethalin 456 g/l), Fist 50 EC, (Pendimethalin 500 g/l).
Zinatumikaje ?
Baada ya kupandikiza vitunguu unapima kiuagugu hiki kiasi cha 100 โ€“ 200 ml kwa bomba lita 20 kisha unapulizia kwenye udongo baada ya kupanda vitunguu, wakati wa kupulizia ni lazima udongo uwe na unyevu wa kutosha. Haina madhara kabisha kwenye vitunguu. Pulizia kabla ya magugu kuanza kuota mara tu baada ya kuotesha,isipite siku 7 maana magugu yataanza kuota.
โžข Volacet 900 EC_ (acetochlor 900 g/l)


Inatumikaje ?
Baada ya kupandikiza vitunguu unapima kiuagugu hiki kiasi cha 100 โ€“ 150 ml kwa bomba lita 20 kisha unapulizia kwenye udongo baada ya kupanda vitunguu, wakati wa kupulizia ni lazima udongo uwe na unyevu wa kutosha. Haina madhara kabisha kwenye vitunguu. Pulizia kabla ya magugu kuanza kuota mara tu baada ya kuotesha,isipite siku 7 maana magugu yataanza kuota.
B)Viuagugu vinavyopulizwa baada ya magugu kuota na vitunguu vikiwa tayari vimeshapandwa.
โžข Pantera 40 EC (Quizalofop-P-Tefuryl 40 g/l) : Kipimo : 60-150 ml/20 L
Muda muzuri wa kupulizia:
PANTERAยฎ 40 EC hufanya kazi vizuri inapopuliziwa kwenye majani yanayokuwa na yasiwe na shida ya unyevu.Kama unalenga nyasi za muda mfupi, unatakiwa usubiri nyasi ziote vizuri lakini uziue kabla majani hayajaanza kushindana na mazao.
Lazima usubiri wiki 2-3 baada ya majani kuota au 60% ya majani yote yanapokuwa yameota. Muda muzuri ni pale nyasi changa zinapokuwa na majani 5-6 katika hatua ya ukuwaji. Kwa majani jamii ya Cynodon dactylon lazima upulize wakati pingili za nyasi zinakuwa na urefu wa 5-15 sm.
NB. Hii inaua nyasi tu (magugu yenye majani membamba tu) kwa hiyo kabla ya kiuitumia inashauriwa ukague shamba lako kujua aina ya magugu, kama asilimia kubwa ni nyasi ndio uitumie ila kama mengi ni yenye majani mapana basi usiitumie.


โžข Centurion 120 EC (Clethodim 120 g/l)
Kipimo : 100 ml /20 L Centurion 120 EC hufanya kazi vizuri inapopuliziwa kwenye majani yanayokuwa na yasiwe na shida ya joto au unyevu.Kama unalenga nyasi za muda mfupi,unatakiwa usubiri nyasi ziote vizuri lakini uziue kabla majani hayajaanza kushindana na mazao.Lazima usubili wiki 2-3 baada ya majani kuota au 60% ya majani yote yanapokuwa yameota. Muda muzuri ni pale nyasi changa zinapokuwa na majani 5-6 katika hatua ya ukuwaji.


Kwa majani jamii ya Cynodon dactylon lazima upulize wakati pingili za nyasi zinakuwa na urefu wa 5-15 sm.
NB . Hii inaua nyasi tu (magugu yenye majani membamba tu) kwa hiyo kabla ya kiuitumia inashauriwa ukague shamba lako kujua aina ya magugu, kama asilimia kubwa ni nyasi ndio uitumie ila kama mengi ni yenye majani mapana basi usiitumie.


Magonjwa na wadudu waharibifu wa vitunguu
Wadudu
Vithiripi (Onion thrips)
Hawa ni wadudu waharibifu namba moja wa zao la vitunguu hapa nchini Tanzania. Husababisha upotevu mkubwa wa mavuno. Wadudu hawa huonekana hasa wakati wa kipindi cha joto/kiangazi
Dalili za kugundua
Majani yaliyo shambuliwa na wadudu hawa huwa na mabaka meupe yenye kung’aa. Katika hali iliyo kithiri majani yote hugeuka kuwa na rangi nyeupe au kijivu cheupe na baadaye majani hunyauka kabisa. Dalili nyingine kubwa ni majani hujikunja. Wadudu hawa huanza kushambulia katikati ya shina/majani ya kitunguu.

Kudhibiti.
Inashauriwa kukagua mara kwa mara na ukiona wadudu hawa wameanza basi anza kupuliza viuadudu haraka iwezekanavyo. Dawa/viuadudu ambavyo vinafanya vizuri sana kuua wadudu hawa ni;
1) TRIUMPH 692 EC (Acetamiprid 32 g/l + Lambdacyhalothrin 60 g/l + Profenofos 600 g/l)
Faida kubwa ya kiuadudu hiki.

 • Ina viambata amilifu 3, vinavyoonekana hapo juu, viambata hivi kila kimoja kina uwezo wa kuua vithiripi wa vitunguu kwa kiasi ila unapozichanganya pamo kama ilivyo kwa Triumph basi ufanisi unaongezeka maradufu.
 • Ina uwezo wa kuua wadudu aina zote wanoshambulia zao la vitunguu, kwa hiyo hata kama shambani kwako kuna aina ya wadudu wengine basi ukitumia TRIUMPH 692 EC wadudu wote watakufa.
 • Huduma kwa muda mrefu, baada ya kuua wadudu hao, hutoa kinga kwa muda siku 14 mdudu hawezi kugusa endapo utakua umepulizia vizuri.
  Kipimo . 10-20ml/ 20 L
  2) Kiuatilifu (dawa) kingine ambacho hufanya vizuri kwa vithiripi wa vitunguu ni;
  Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l)
  -Pia inaua wadudu wote kwenye zao la vitunguu.
  -Hutoa kinga mpaka siku 14 bila mdudu kugusa endapo utapulizia vizuri.
  Kipimo : 10-20 ml/20 L
  3) Crotale 46 SC (Indoxacarb 30 g/l + Acetamiprid 16 g/l)
  -Pia inaua wadudu wote kwenye zao la vitunguu.
  -Hutoa kinga mpaka siku 14 bila mdudu kugusa endapo utapulizia vizuri.
  Kipimo: 20 – 40 ml/20 L
  NB : Inashauriwa usipulizie kiuadudu aina moja kwa muda mrefu, tumia Triumph na cutter au Crotale kwa kubadilishabadilisha, yaani mfano leo ukipulizia Triumph siku nyingine unapopulizia tumie Cutter na baadaye rudia Triumph na endelea na mzunguko huo, inashauriwa hivyo kuepuka usugu wa kiuatilifu/ wadudu kuzoea kiuadudu
  Kumbuka :
  Majani ya vitunguu huteleza sana na hivyo kiuadudu kuna muda kinaweza kisifanye kazi vizuri kwa hiyo inashauriwa kutumia vinatisha viuatilifu kama vile Wet all, Spray firm, Silwet gold.Hivi hufanya dawa/kiuadudu kinate kwenye jani na hivyo huongeza ufanisi wa kiuadudu.
  Wadudu wengine.
  Wadudu wengine waosumbua sana kwenye zao la vitunguu ni Katapila/funza, wako wa aina nyingi.Ambo ni shida kubwa na hasa maeneo ya Ruaha mbuyuni kwa kiswahili tunawaita ng’onyo. Ni funza ambao hukata miche/vitunguu kwa chini kwenye shina, karibu na udongo na wadudu hawa hukata muda wa jioni.
  Uwadhibiti.
  Tumia hivyo viuatilifu nilivyotaja hapo juu, kingine ambacho ni kizuri sana kwa hawa wadudu ni
  *Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/l + Acetamiprid 16 g/l)
  Hiki kiuatilifu kingine hatarii sana kwa wadudu, huua pia wadudu wote kwenye zao la kitunguu.

Uwadhibiti.
Tumia hivyo viuatilifu nilivyotaja hapo juu, kingine ambacho ni kizuri sana kwa hawa wadudu ni
*Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/l + Acetamiprid 16 g/l)
Hiki kiuatilifu kingine hatarii sana kwa wadudu, huua pia wadudu wote kwenye zao la kitunguu.
*Kipimo 20-40ml/20 L
NB Kwa vile ng’onyo/funza/katapila hukata vitunguu/miche mida ya jioni, inashauriwa upulizie dawa/kiuadudu mida ya jioni sana na ikiwezekana usiku kabisa.
Hitimisho
Kwa leo tutaishia hapa, kesho tutaendelea na mbolea na kesho kutwa magonjwa au vyote kesho. Ahsanteni sana, sasa karibuni kwa maswali.
Swali1: Mimi NAOMBA kuuliza swali la jumla ekari MOJA ya KILIMO cha VITUNGUU kuanzia kuandaa SHAMBA hadi kuvuna inachukua GHARAMA gani
Agronomist Peter Jibu1: Tsh 3 million inatosha, gharama hizi zinaweza kupungua au kuongezeka kutokana na sababu tofautitofauti kama vile upatikanaji wa vibarua, maji yanatoka wapi na unatumia nini kuvuta maji, nk
Swali2: Asante kwa somo, vipi kama thrips wameshambulia sana ili kuwadhibiti dawa nipulize kwa interval ya siku ngapi? ili kuwatokomeza kabisa
Jibu2: Baada ya siku 5-7 rudia na baada ya hapo unaweza kaa hadi siku 14 ila kukagua shamba mara kwa mara ni mhimu sanaaaa.
Swali3: Ubarikiiwe Kaka peter na Nimeipenda hii dawa, Nina swali vipi pale unaposia mbegu kwnye kitalu Kuna sawa ya magugu maalumu ya kupiga kwenye kitalu Cha kitunguu?
Jibu3: Hizo za nyasi magugu yakiota aina ya nyasi unaweza kuzitumia. Ila hizo za kuzuia majani kuota nashauri kwenye kitaru zisitumike.
Magonjwa makuu kwenye zao la kitunguu nchini Tanzania.
1) Ubwiri chini (Onion Downy Mildew )
โœ“ Huu ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi.
โœ“ Hushamili sana wakati wa baridi kali, ukungu na kwenye udongo ambao maji yanatuama kwa muda mrefu (soi with poor drainage condition)
Dalili kuu za huu ugonjwa
โœ“ Kwenye ncha za majani yaliyokomaa huwa na michilizi ya njano, kukauka, kusinyaa na kuwa na rangi brauni au njano na baadaye kufa kwa mmea.
Kudhibiti.
โœ“ Zingatia usafi wa shamba.
โœ“ Lima kwa kubadili mazao (Crop rotation)
โœ“ Tumia viuakuvu/vizuiakuvu.
Viuakuvu vinavyoweza kutibu na kuzuia ugonjwa huu.
โœ“ Evito T477 SC (fluoxastrobin 200 g/l + tebuconazole 277 g/l)
โœ“ Ivory M 72 WP (mancozeb 640g/Kg + Metalaxyl 80g/Kg
โœ“ Tridium 700 WG (Azoxystrobin 47 g/kg + Mancozeb 597 g/kg + Tebuconazole 56 g/kg)
โœ“ Glory 750 WG (Azoxystrobin 50 g/kg + Mancozeb 700 g/kg)
Viuakuvu vinavyoweza kuzuia/kinga tu
โœ“ Banko 720 SC (chlorothalonil 720 g/l)
โœ“ Banko 500 SC (chlorothalonil 500 g/l)
โœ“ Cuprocaffaro 50 WP (copper oxychloride 500 g/kg)
โœ“ Ivory 80 WP (mancozeb 800 g/Kg)
โœ“ Uthane 80 WP (Mancozeb 800 g/kg)

2) Purple Blotch
Ugonjwa huu pia husababishwa na fangasi pia.
Dalili .
โœ“ Madoadoa kama meupe kwenye majani.
โœ“ Hushamili sana maeneo yenye baridi na unyevu mwingi.
โœ“ Madoadoa hayo madogo meupe ndani ya muda mfupi huwa makubwa na kubadili rangi kuwa kama papo na pembeni ya hilo doa huwa na rangi kama ya njano au orenji
โœ“ Doa hilo hukua na baadaye hupelekea jani kufa.
โœ“ Ugonjwa huu huweza kuenea mpaka kwenye kitunguu chenyewe (onion bulb) na kusabaisha kuoza kwa kitunguu ambapo huanza kuoza kuanzia kwenye shingo la shina.
Kudhibiti.
โœ“ Zingatia usafi wa shamba
โœ“ Lima kwa kubadili mazao (crop rotation)
โœ“ Baada ya kuvuna toa masalia yote shambani.
โœ“ Panda kwa umbali unaotakiwa kuepuka umande kuwa mwingi.
โœ“ Tumia viuakuvu.
Viuakuvu ambavyo huweza kutibu na kuzuia ugongwa huu.
โœ“ Eminent Star (chlorothalonil 250 g/l + tetraconazole 62.5 g/l)
โœ“ Evito T477 SC (fluoxastrobin 200 g/l + tebuconazole 277 g/l)
โœ“ Ivory M 72 WP (mancozeb 640g/Kg + Metalaxyl 80g/Kg
โœ“ Tridium 700 WG (Azoxystrobin 47 g/kg + Mancozeb 597 g/kg + Tebuconazole 56 g/kg)
โœ“ Glory 750 WG (Azoxystrobin 50 g/kg + Mancozeb 700 g/kg)
Viuakuvu vinavyoweza kuzuia/kinga tu
โœ“ Banko 720 SC (chlorothalonil 720 g/l)
โœ“ Banko 500 SC (chlorothalonil 500 g/l)
โœ“ Cuprocaffaro 50 WP (copper oxychloride 500 g/kg)
โœ“ Ivory 80 WP (mancozeb 800 g/Kg)
โœ“ Uthane 80 WP (Mancozeb 800 g/kg)
โœ“ Devisulphur 800 WG (Sulphur 80%)

Hizo ni picha zinazoonyesha purple blotch kwenye vitunguu.

3) Kutu (Rust)
Ugonjwa huu pia husababishwa na fangasi, hushamili sana maeneo yenye joto na kiwango cha
maji kwenye hewa kinapokua kingi (Humidity)
Dalili:
โœ“ Madoadoa madogomadogo yenye rangi kama nyekundu kuonekana kwenye majani ya kitunguu
โœ“ Majani yaliyoathiriwa sana hubadilika na kuwa rangi ya njano na baadaye kufa kabla ya kitunguu kukomaa.
Kudhibiti.
โœ“ Zingatia usafi wa shamba
โœ“ Hakikisha mimea yako inapataka chakula cha kutosha (mbolea)
โœ“ Tumia viuakuvu.
Viuakuvu ambavyo hufanya vizuri kwa huu ugonjwa ni;
โœ“ Evito T477 SC (fluoxastrobin 200 g/l + tebuconazole 277 g/l)
โœ“ Tridium 700 WG (Azoxystrobin 47 g/kg + Mancozeb 597 g/kg + Tebuconazole 56 g/kg)
โœ“ Glory 750 WG (Azoxystrobin 50 g/kg + Mancozeb 700 g/kg)
โœ“ Eminent Star (chlorothalonil 250 g/l + tetraconazole 62.5 g/l)

Hizo picha zinaonyesha ugonjwa wa kutu ya majani kwenye vitunguu. Ugonjwa huu hupenda sana vitunguu swaumu zaidi ya vitunguu maji.

4) Kuoza singo la kitunguu (Neck Rot)
Ugonjwa huu mara nyingi huonekana baada ya kuvuna, ukihifadhi vitunguu. Husababishwa na fangasi pia ambao huingia kwenye kitunguu kupitia kidonda au mpasuko kwenye
kitunguu.
Dalili : Angalia picha.
Kudhibiti:
โœ“ Tumia chanjo ya mbegu (seeds treatment) kabla ya kupanda, nzuri sana ni seedplus
30 WS
โœ“ Epuka kuumiza vitunguu wakati wa kuvuna.
โœ“ Usilazimishe vitunguu vikauka kwa kulaza mashina ili uwahi kuvuna, kufanya
hivyo huweza kusabisha vidonda kwenye shingo la vitunguu.
โœ“ Vuna vitunguu wakati vimekomaa vizuri, shingo ya kitunguu vilivyokomaa vizuri
hulala.

Hizo picha zinaonyesha ugonjwa wa kuoza shingo la vitunguu (neck rot), wakulima wengi, vitunguu vinapo karibia kukomaa wamekua wanapitisha pipa juu ya vitunguu, majani/shina la vitunguu hulala. Hufanya hivi ili majani yakauke mapema wavune, hili jambo halishauriwi, kwani kama unaenda kuhifadhi huweza kutokea huo ugonjwa.
MASWALI NA MAJIBU Swali A: Ukivuna..naona wengine hukata majani ya juu manually..je ikiwa large scale unafanyaje ili majani yaishe haraka ili viende sokoni?
Jibu A: Swali zr, hili naomba wengine humu wanisaidie kujibu.
Note.
Ukitaka uhifadhi vitunguu kwa muda mrefu usivikate majani na kama utakata basi acha sehemu kiasi ya shida, angalau 3-5 sm kutoka kwenye kitunguu.
Pia tumia mbolea inayoshauliwa hapo juu shingo itakuwa nyembamba.
Swali B: Mwl swali langu .Wateja wengi wanapenda VITUNGUU vyenye shingo nyembamba. Nifanyeje ILI SHAMBA langu nipate VITUNGUU vyenye shingo nyembamba.
Jibu B: Usiwahi kuvuna, ukisubiri vikomae vizuri shingo itakua nyembamba.

Kwa maelezo Zaidi piga simu No. 0744529070 Agronomist Peter

leave your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Ads
Tsh. 1,800 (Negotiable)
Tsh. 1,500 (Negotiable)
Tsh. 1,000 (Negotiable)
Tsh. 30,000 (Negotiable)
Featured Ads
Top
Translate ยป