For a better experience please change your browser to CHROME, FIREFOX, OPERA or Internet Explorer.
KILIMO BORA NYANYA

KILIMO BORA NYANYA

KILIMO CHA NYANYA
UTANGULIZI

Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Na kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zao la nyanya ndio zao namba moja linaloweza kutoa pesa nyingi ukilinganisha na mazao mengine ya mbogamboga. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Nyanya ni jamii ya mazao ya Solanaceae, mazao mengine marufu katika kundi hili ni pilipili hoho, biringanya, ngogwe na viazi mviringo. Uzalishaji wa nyanya unahitaji uangalizi na matunzo ya hali ya juu katika huduma ya pembejeo. Pamoja na hayo zao hili linaweza kumpatia mkulima faida kutokana na mahitaji yake katika matumizi ya kila siku kwenye familia za aina zote.
Hali ya hewa
Nyanya hustawi vizuri kwenye hali ya hewa yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 21 na 32 C na katika mwinuko wa mita 300-1400 juu ya usawa wa bahari na huhitaji maji mengi kiasi cha mm 1800 kwa msimu.
Udongo
Udongo tifutifu wenye rutuba ya kutosha usiotuamisha maji hufaa zaidi kwa kilimo cha nyanya, japo kuna uwezekano wa nyanya kuzalishwa hata katika udongo wenye kichanga au mfinyanzi. Kiwango cha tindikali na chachu katika udongo ( Soil pH) kinapaswa kudhibitiwa. Nyanya hustawi vizuri kwenye pH ya kati ya 5.5 โ€“ 75 lakini hustawi vizuri zaidi kwenye pH ya 6-6.5 (Soil pH)
Aina za nyanya
Kuna aina kuu mbili za nyanya
Nyanya zinazokuwa ndefu (Indeterminate)
Aina hii ya nyanya huendelea kukua na kuzaa kwa muda mrefu. Hutolewa machipukizi au maotea na kubaki shina moja au matawi mawili tu. Husegekwa kwa kutumia miti mirefu, kamba ndefu na wakati mwingine nyaya hutumika.Nyanya aina hii na mahususi kwa kilimo katika mabanda (greenhouse). Mkulima anaweza kulima aina hii ya nyanya nje lakini anahitaji kuwa na nguvu kazi kubwa kwa ajili ya kuweka miti. Ukiilima ndani unaweza vuna kwa muda usiopungua miezi 9 na iwapo utailima nje unaweza vuna kwa muda usiopungua miezi 6 mfululizo.Mfano wa mbegu hii ni ; Anna F1, Tylka F1, Eva F1, Uwezo, Moyo, nk.

Nyanya ndefu katika banda ( green house)
Nyanya fupi ( Determinate)

Hizi ni nyanya fupi, zinakuwa na kikomo cha kukua ndani ya muda mfupi. Huvunwa kwa muda mfupi, kiasi cha miezi 2-4 tu.Ni nyanya zinazoshauriwa kulimwa kibiashara na wakulima wenye mashamba makubwa. Aina hii ya nyanya aipogolewei machipukizi na huwekewa miti mifupi ya kiasi cha mita 1.5-2. Mfano wa aina hii ya mbegu ni Kilele F1, Asila F1, Edeni F1, Nuru F1, Monica F1, Jara F1, Tanya, Mwanga, Riogrand, Imara nk. Mbegu hizi hupatikana kwenye makampuni mbalimbali mfano Mosanto, Rijz zwaan, Balton, syngenta, Royal seeds, kibo seed, East Africa na wengineo wana mbegu aina mbalimbali na nzuri.
NB: Aina hizo mbili za nyanya pia zimegawanyika; kuna mbegu chotara (Hybrid) na mbegu zilizoboreshwa (OPV) na mbegu chotora ndio mbegu nzuri zaidi.
Mfano wa mbegu chotara (Hybrid) ni;
Asila f1, Anna F1, Kilele F1, Edeni F1, Nuru F1, Rambo F1, Monica F1, Milele F1, Jara F1, Tylka F1, Kipato F1, Shanty F1, Imara, nk
Mfano wa mbegu za kawaida zilizoboreshwa ni;
Tanya, Rio Grande, Onyx, Tengeru 97, Mwanga, nk
Mahitaji ya mbegu.
Ni muhimu kutumia mbegu bora kila wakati. Kiasi cha gramu 50-100 ya mbegu hutosha kupanda ekari moja kutegemea njia usiaji, uotaji na nafasi ya kupanda. Mbegu ya nyanya huota baada ya siku 4-8.

Nyanya Fupi, nanenane, 2014- Morogoro Tz. Ilisimamiwa na Agronomist Peter akiwa Syngenta wakati huo.

Kusia/vitaru.
Kuna aina mbili kuu ya vitaru, vitaru sinia ( Tray) na vitaru vya chini. Vitaru sinia ni vizuri sana kwani husaidia kuepuk magonjwa ya ardhini na ukitunzia miche kwenye vitaru sinia miche hukua vizuri na kwa haraka zaidi.
Vitaru vya chini pia vimegawanyika, kuna vitaru mbinuko na vitaru mbonyeo. Vitaru mbinuko ni vizuri kwani husaidia hewa kuzunguka kwa urahisi.
Kwa kawida miche nyanya huwa tayari kupandikizwa shamba kubwa baada ya siku 21 tangia kumwaga mbegu chini/kusia.

Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa kina cha sentimita 30-45 na kisha andaa matuta yenye upana wa sentimita 150 kutoka katikati ya tuta moja na lingine.Unaweza lima bila matuta lakini zipo faida zitokanazo na matumizi ya matuta katika kilimo, baadhi ya faida hizo ni kuwa matuta huweza kuruhusu mizizi kusambaa vema na kupata virutubisho, unyevu na hewa. Matuta pia huondoa maji mengi yaliyozidi shambani hasa wakati wa mvua nyingi.
Upandaji.
Nyanya hupandwa kwa umbali wa nafasi ya sentimita 30 mche na mche na sentimita 60 mstari na mstari ( kwa mbegu za kawaida zilizoboreshwa). Kwa mbegu chotara inshauriwa mche na mche iwe sentimita 60 na mstari na mstari iwe sentimita 90.
Panda kwa kutumia mbolea kianzio (starter solution), tengeneza mwenyewe hiyo mbolea kwa kutumi DAP ( Chukua 3 Kg za DAP na weka kwenye maji lita 200, hii ndio ratio, hakikisha wakati wa kuweka stater haigushi majani ya miche)


Uwekaji miti /usegekaji
Nyanya ni mimea nyenye shina laini lisiloweza kusimama wima bila usaidizi, hivyo basi ili kuweza kuongeza uzalishaji kwa kuepuka magonjwa ni muhimu mimea ya nyanya iweze kuwekewa miti ili isimame imara bila kutambaa ardhini. Zipo aina nyingi za uwekaji miti kutegemea na aina ya nyanya, kama ni fupi au ndefu na pia hutegemea na upatikanaji wa vifaa kama vile miti/fito, waya, nk.


Uwekaji miti hupunguza mashambuzi ya magonjwa na wadudu kwa kuruhusu mzunguko wa hewa kupita vema na kuongeza ukuaji mzuri kwa kuruhusu mwanga kupenya kwa urahisi. kwa ekari moja inahitaji miti 1800 urefu ni mita 1.5 โ€“ 2 na kamba mita 15000 ambayo itakuwezesha kufunga mizunguko mitatu weka mita kwa muda muafaka kabla ya kupanda au baada ya kupanda na isizidi siku 14 na mti na mti weka cm 150 usipungue hapo watu wengi hukosea hapa wanaweka sm 200 au 300 na mimea ina anguka kwa hiyo maana ya kufunga kamba inakuwa haipo.


Kupunguza machipukizi/ Maotea na majani
Ni muhimu kwa nyanya ndefu kuondoa machipukizi na kabakia shina moja au mawili tu ili kupunguza msongamano na hivyo mimea huzaa matunda yenye ubora wa kutosha. Kwa nyanya fupi hakuna sababu ya kupunguzia lakini majani hupunguzwa matunda yanapokaribia kokomaa.

Palizi
Magugu hushindana na mazao katika kugombea virutubisho, mwanga, hewa na unyevu. Magugu ni moja ya visumbufu kwa mazao yetu. Shamba lililojaa magugu huvutia wadudu na vimelea vya magonjwa kuweza kujificha na kufanya mashambulizi kwa mazao hivyo shart yaondolewe na kuacha shamba likiwa katika hali ya usafi kila wakati. Zipo njia kadhaa za udhibiti wa magugu shambani, kama palizi, kungโ€™oa kwa mkono, kutumia viuagugu kabla na baada ya kupanda, kabla ya kupanda kama shamba lina majani unashauriwa kutumia viuagugu vinavyoua magugu yote mfano wa viuagugu hivo ni ;
โžข Kalach 480 SL (Glyphosate 360 g/โ„“ (480 g/โ„“ as IPA salt), Kipimo: 1 – 6 โ„“/ha (or 80 – 480 mโ„“ kwa bomba 20 L kulingana na aina ya magugu na ukubwa wa magugu. Pulizia wakati magugu yapo kwenye hali ya ukuaji, yasiwe yameanza kukauka na kama magugu ni makubwa tumi kipimo kikubwa kinachoshauriwa.
โžข Volsate 360 SL (Glyphosate 360 g/โ„“ (480 g/โ„“ as IPA salt) Kipimo: 1 – 3 โ„“/ha (or 80 – 240 mโ„“ kwa bomba 20 L

NB: Usitumie viuagugu hivi kama tayari umeshapanda, vitaua mimea yako.
Viuagugu ambavyo huweza kuua magugu na nyanya zikabaki ni:

โžข Pantera 40 EC (Quizalofop-P-Tefuryl 40 g/โ„“): Kipimo: 1 โ€“ 3 โ„“ /ha (au 80 – 320 mโ„“ per 20 L, tumia kipimo kikubwa kama magugu/majani ni makubwa.
โžข Centurion 120 EC (Clethodim 120 g/โ„“): Kipimo: 1 โ€“ 2 โ„“/ha (au 80 – 160 mโ„“ kwa bomba 20 L


NB: Viuagugu hivi huua magugu aina ya nyasi tu, kama kuna magugu/majani yenye majani mapana hayatakufa na hivyo unashauriwa kukagua shamba lako kuangalia aina ya magugu na kama mengi ni nyasi ndio utumie hivi viuagugu tofauti na hapo usitumie.


Mbolea.
Nyanya kama yalivyo mazao mengine huhitaji rutuba ya kutosha yenye virutubisho mbalimbali kama vile naitrojeni, fosforasi, potasium, manganizi, kalshamu n.k. Virutubisho hivyo vinahitajika kwa kiwango na wakati tofauti na hufanya kazi tofauti kwa mmea, kwa hiyo ni muhimu kuweka mbolea zenye virutubisho vyote na kwa wakati muafaka ili kupata mazao bora.


Unapopanda nyanya anza na starter iliyotengenezwa kutoka kwenye DAP, kutengeneza hiyo starter changanya 3 kg ya DAP kwenye maji lita 200 na kisho weka 250 ml kwa kila shina, hakikisha maji ya mbolea hiyo hayagusi majani.
Baada ya hapo, subili siku 5-7 na weka DAP au Yara otesha au NPK, kiasi cha 5g kwa kila shina na baada ya siku 21 tangia uweke DAP weka Yalamira winner/NKP kiasi cha 5g kwa shina, baada ya siku 14-21 tangia uweke yalamila winner weka Yalavita nitrabo au CAN kiasi cha 5 โ€“ 10g kwa kila shina. Baada ya kuweka mbolea hizi subili siku 21 na weka MOP kiasi cha 5 -10 g kwa kila shina na endelea kuweka CAN, NPK NA MOP kwa kubadili kila baada ya siku 21 hadi mwisho wa mavuno.
Madini ya Naitrogen (N)
Ni madini muhimu kwa ajili ya ukuaji, hasa utengenezaji wa majani ya rangi ya kijani kibichi. Madini haya huhitajika sana wiki chache baada ya kupandikiza. Rangi ya kijani ni muhimu kwa ajili ya utengenezaji wa chakula cha mimea. Kunapokuwa na upungufu wa naitrogeni, rangi ya majani hupauka kuwa njano na mimea hudumaa. Hata hivyo, haifai kutumia naitrojeni nyingi
kupita kwani ikizidi, mimiea huwa na majani mengi bila matunda na hivyo kuathiri mavuno Panapokuwa na upungufu wa naitrojeni, inashauriwa kutumia mbolea za chumvi kama CAN, UREA, SA na NPK.

Dalili za upungufu wa naitrojeni, majani kuwa njano

Fosforasi (P)
Ni madini muhimu kwa utengenezaji wa mizizi na matunda kwa mimea na huhitajika mara moja wakati wa kupanda. Inapatikana katika mbolea aina ya Minjingu, DAP, TSP, NPK n.k. Madini haya pia haipaswi kutumika kwa wingi kupita kiasi kwani ikitumika kupita kiasi huzuia mimea kuchukua kutoka ardhini madini joto aina ya zinki. Ili kutambua upungufu wa kirutubisho cha fosforasi katika mimea, rangi ya majani na shina hubadilika na kuwa rangi ya zambarawe hasa sehemu za pembeni, ncha huonekana kama zimeungua na yale majani ya chini hubadilika na kuwa ya kahawia na mwisho hudondoka.


Upungufu wa fosforasi, majani na shina huwa zambarawe
Madini aina ya Potashi (K)

Ni muhimu wakati wa maua, matunda kwa mmea na kuimarisha ubora wa mbegu. Madini ya potash pia huimarisha kinga ya mimea dhidi ya mashambulizi ya magonjwa mbalimbali . Upungufu wa madiniya potash huambatana na dalili kama vile majani kuonekana kama yamebabuka kwa moto sehemu za pembeni na majani kuwa ya njano katikati ya mishipa yake na pembeni. Dalili hizi huanza katika majani ya chini ya mmea na kupanda juu. Dalili katka matunda yanapoiva ni kupauka na kutokuwa na rangi nyekundu iliyokolea.

Dalili za upungufu wa potash katika majani na katika tunda.

Madini ya Magnesiam (Mg)
Ni madini muhimu katika kuhakikisha ubora wa matunda . Dalili za upungufu wa madini haya ni pamoja na majani kuwa na unene na uzito kupita kiasi. Dalili nyingine za upungufu wa magnesiam ni mishipa katika majani hupoteza rangi asilia ya kijani iliyokolea na kuwa na rangi iliyopauka. Upungufu hutokea hasa katika udongo wenye kichanga na tindikali nyingi na pia katika udongo wenye maji kupita kiasi na katika hali ya ukame mkali.Panakuwa na upungufu wa madini haya, inashuriwa kutumia mbolea zenye madini haya kama magnesium sulphate.

Dalili za upungufu wa magnesiam katika majani.

Madini chokaa ya kalisi (Ca)
Nyanya ni zao linalohitaji sana madini haya. Endapo madini haya yatapungua, vitako vya matunda ya nyanya hubadilika rangi na kuwa nyeusi na kisha husinyaa na kuoza. Aina mbalimbali za nyanya pia hutofautiana katika mahitaji ya madini haya kwani zipo aina zinahitajika kwa wingi sana na hizo huathirika zaidi panapokuwa na upungufu. Inashauriwa kutumia mbolea aina ya calcium nitrate na kusambaza chokaa shambani ili kuinua kiwango cha madini haya panapokuwa na upungufu. Pia mwagilia kwa wakati, calcium husafiri kupitia njia ya maji na hivyo panapokuwa na umwagiliaji usiokua na mpangilio huathili pia upatikanaji wa calcium, pia hakikisha ardhi yako imelimwa vizuri kuhakikisha mizizi inapenya vizuri ardhini.

Dalili za upungufu wa chokaa (calcium)

Angalizo: Kabla ya kutumia aina yoyote ya mbolea, ni vema kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu aina, kiasi, namna na wakati wa kutumia. Inapobidi ni vema kupima udongo kujua virutubisho vilivyopo na kiasi chake pamoja na tindikali (Soil pH) na kiwango cha chumvi (EC) katika udongo.

Umwagiliaji

Nyanya ni zao linalohitaji maji mengi hasa wakati wa kupandikiza, wakati wa kutoa maua na wakati wa kutoa matunda. Ni muhimu pia kuwa na uwianao mzuri wa umwagiliaji muda wote badala ya umwagiliaji usiotabirika. Kunapokuwa na maji kidogo wakati wa matunda, matatizo kama upungufu wa madini ya kalisi hujitokeza sana hata kama katika udongo hakuna upungufu wa madini hayo. Hii inatokana na ukweli kwamba madini ya kalisi huhitaji maji mengi ili kuyeyuka na kuweza kufyonzwa na mimea. Dalili za upungufu wa maji hupelekea upungufu wa madini ya kalisi na katika nyanya matunda kuoza katika kitako na kuwa na rangi nyeusi. Kuna umwagiliaji wa matone, mifereji, n.k.

Matandazo

Matandazo ya masalia ya mpunga, mahindi, mtama, migomba pamoja na nyasi kavu hutumika kufunika udongo shambani ili kupunguza upotevu wa unyevu. Matandazo husaidia pia kudhibiti magugu na pindi yanapoozo huongeza rutuba ya udongo (mboji). Matandazo huweka uwiano mzuri wa joto la udongo la udongo na huwa chachu ya kuzaliana kwa wadudu muhimu (fauna na flora) katika kuboresha uhai wa udongo kama vile minyoo ardhi n.k.
Muzunguko wa Mazao
Kilimo cha mzunguko wa mazao ni muhimu kuzingatiwa wakati wote kwani husaidia kudhibiti maambukizi ya wadudu na magonjwa kwa mazao. Mzunguka wa mazao pia hutoa fursa kwa matumizi sahihi ya ardhi na udongo kutokana na ukweli kuwa mazao hutofautiana katika mahitaji na matumizi ya madini ardhini bali pia yapo mazao ambayo husaidia katika kurutubisha udongo. Hivyo inashauriwa kubadili nyanya na jamii yake kila baada ya msimu. Mazao ya jamii ya nyanya ni kama vile, pilipili, biringanya, ngogwe, viazi mviringo n.k. Ili kuwa na mzunguko bora wa mazao katika shamba la nyanya waweza kulima kwa kubadilisha na kabichi, vitunguu, maharage, karoti n.k.
Wadudu
Nzi weupe (Whitefly)

Ni wadudu waupe wadogowadogo wanao fanana na nzi na huruka unapotikisa mmea. Wadudu hawa hushambulia kwa kufyonza majimaji ya majani, hasa majani machanga. Mbali na kufyonza majimaji ya mimea huambukiza magonjwa ya virusi ambayo ni hatari na hayana tiba.


Nzi weupe
Udhibiti

Tumia viuatilifu vinavyoshauriwa na wataalamu. Usafi wa shamba na uondoaji wa masalia ya mazao na kuyachoma mara moja baada ya mavuno hupunguza kuzaliana kwa wadudu hawa na hivyo kupunguza mashambulizi.
Viuadudu ambavyo hufanya vizuri kudhibiti wadudu hawa ni:
โžข Evisect 50 SP (Thiocyclam 50 %): Kipimo: 500 โ€“ 750 g/ha (or 25 g / 20 L. Hii ndio kiuadudu bingwa No.1 kwa hawa wadudu, unapopulizia hakikisha kila jani linashika kiuadudu na rudia kupulizia kila baada ya siku 7 โ€“ 14 kama wadudu bado wapo, kagua mimea yako kabla ya kupulizia.
โžข Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/โ„“ + Lambdacyhalothrin 60 g/โ„“ + Acetamiprid 32 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Uniron 100 EC (Novaluron 100 g/โ„“): Kipimo: 350 mโ„“/ha (au 20 mโ„“ / 20L
โžข Thiamex 250 WG (Thiametoxam 250 g/kg): Kipimo: 600-800 g/ha (or 12-16 g /20 โ„“
Utitiri mwekundu (Redspider mites)
Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi nyekundu. Hujilinda kwa utando kama buibui wafanyavyo. Hawa hufanya uharibifu kwa kula majani hivyo majani huwa na madoa madoa madogo yenye rangi ya njano. Wadudu hawa pia hula matunda na kusababisha michubuko midogo midogo yenye rangi ya njano au nyeupe iliyofifia.

Utitiri mwekundu/ yebo yebo ( Red spinder mites)
Udhibiti

Tumia viuatilifu kwa kufuata maelekezo ya wataalamu, Usafi wa shamba na mazingira yake hasa kwa kuondoa magugu ya jamii ya nyanya kama vile ndulele na mnafu karibu na shamba hupunguza mazalia. Matumiza ya makingo hai pia hunguza mashambulizi kutoka katika mashamba ya jirani. Wadudu hawa huathiri sana wakati wa kiangazi na pia hupendelea sana ndani ya banda (green house)
Baadhi ya viuatilifu vinavyodhibiti wadudu hawa ni:
โžข ABALONE 18 EC (Abamectin 18g/l): Kipimo: 250- 500 mโ„“/ha au 10 – 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข FLORAMITEยฎ 240 SC (bifenazate 240 g/L): Kipimo: 10 mโ„“/20 L

Wadudu mafuta/kimamba (Aphids)
Hawa ni wadudu wanaofyonza majimaji kwenye majani. Wana rangi mbalimbali kama vile nyeusi, kijani, njano, n.k. na huwa mbawa. Kama walivyo nzi weupe, wadudu mafuta pia husambaza magonjwa ya virusi na pia husababisha unato unaosababisha ugonjwa wa masizi (soot mold) ambao hutanda na kuweka rangi nyeusi kwenye majani ya mimea, matunda na hata matawi.

Wadudu mafuta kwenye majani ya nyanya.

Udhibiti
Tumia viuatilifu kwa kufata maelekezo ya wataalam.
Viuadudu ambavyo hudhibiti vizuri hawa wadudu ni:
โžข Attakan C 344 SE (Imidacloprid 200 g/โ„“ + Cypermethrin 144 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“ /ha (au 20 mโ„“ / 20 L -Huyo ndio bingwa No. 1
โžข Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/โ„“ + Lambdacyhalothrin 60 g/โ„“ + Acetamiprid 32 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/โ„“ + Acetamiprid 16 g/โ„“): Kipimo: 1โ„“/ha au 20 โ€“ 40 mโ„“
Funza wakataji (Cutworms)
Funza hawa ni wafupi na wanene hukaa ardhini. Wanaposhikwa na kuwekwa kiganjani, hujikunja na kuwa mviringo. Wakati wa mchana hujificha ardhini na huibuka wakati wa usiku na kukata mimea michanga hasa wakati wa kupandikiza Mashambulizi makubwa huonekana katika mashamba yenye magugu, yenye mboji nyingi na hasa wakati wa mvua. Funza hawa hushambulia nyanya kabla ya kuanza kutoa matunda.

Funza wakataji ( Cutworms)

Udhibiti
Tumia viuatilifu kwa maelekezo ya wataalamu.
Baadhi ya viuatilifu vinavyofanya vizuri kuua hawa wadudu ni:
โžข Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/โ„“ + Lambdacyhalothrin 60 g/โ„“ + Acetamiprid 32 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/โ„“ + Acetamiprid 16 g/โ„“): Kipimo: 1โ„“/ha au 20 โ€“ 40 mโ„“
NB: Pulizia wakati wa jioni sana au usiku kabisa kama inawezekana.

Funza wa vitumba (American Bollworm)
Hawa pia hushambulia nyanya mara tu matunda yanapoanza. Hutoboa na kuingia katika matunda yanapokuwa madogo. Ni rahisi kuwadhibiti funza hawa wanapokuwa wadodgo lakini pindi wakiwa wakubwa ni vigumu kuwadhibiti na wakati huo pia huwa wameshakwisha kusababisha hasara kwa kutoboa matunda na kuyaozesha


Funza wa vitumba ( American Bollworm)
Viuadudu ambavyo hudhibiti wadudu hawa ni;
โžข Attakan C 344 SE (Imidacloprid 200 g/โ„“ + Cypermethrin 144 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“ /ha (au 20 mโ„“ / 20 L -Huyo ndio bingwa No. 1
โžข Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/โ„“ + Lambdacyhalothrin 60 g/โ„“ + Acetamiprid 32 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/โ„“ + Acetamiprid 16 g/โ„“): Kipimo: 1โ„“/ha au 20 โ€“ 40 mโ„“

Minyoo Fundo (Nematodes)

Ni minyoo wadogo sana ambao huathiri mizizi kwa kuchimba ndani ya mizizi na kusababisha vifundo na mizizi kuvimba. Uvimbe na vifundo huathiri uwezo wa mizizi kunyonya maji na virutubisho katika kutoka ardhini, hivyo miea hudhoofika, hunyauka, hudumaa na kushindwa kuzaa.

Madhara ya minyoo fundo

Udhibiti
Panda aina ya nyanya zinazo stahimili ( Resistant varieties), tumia mzunguko wa mazao kupunguza mashambulizi. Pia unaweza kutumi dawa kama Solvigo 108 SC (Thiamethoxam 72g/l + Abamectin 36g/l), Bio-Nematone 1.15%WP (Paecilomyces Lilacinus 1.15%), Real Trichoderma (Real Trichoderma), Furaban 3GR (Carbofuran 3g/kg), NEMACUR 5 GR (Fenamiphos), PL-Plus (Paecilomyces lilacinus Spores 2 x 109)

Chorachora ( Leaf Miners)
Mabuu ya wadudu hawa hula majani ya nyanya na kutengeneza michirizi kama ramani. Michilizi hii pia huonekana kama machimbo ya mgodi na ndiyo chimbuko la jina la wadudu hawa kwa kiingereza. Michirizi hii hupunguza maji katika majani na hivyo kusababisha kudondoka, hupunguza uwezo wa mimea kutengeze chakula chake na kupunguza mavuno.

Chorachora ( Leafminer)

Baadhi ya viuatilifu vinavyodhibiti wadudu hawa ni:
โžข ABALONE 18 EC (Abamectin 18g/l): Kipimo: 250- 500 mโ„“/ha au 10 – 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mโ„“/ha
au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข FLORAMITEยฎ 240 SC (bifenazate 240 g/L): Kipimo: 10 mโ„“/20 L
Kanitangaze (Tuta absoluta)
Huyu ni mdudu mpya, kwa mara kwanza aliripotiwa Tanzania mwaka 2014. Mdudu huyu
huweza kula majani, shina na matunda, kwa hiyo huweza kusababisha hasara asilimia 100.
Huyu mdudu ni sugu kwa viuadudu vingi, kuna viuadudu maalumu kwa huyu mdudu na hivyo
viuatilifu iwapo utapulizia aina moja mfulilizo kwa muda mrefu,basi kanitangaze huweza
kujenga usugu wa viuadudu husika. Kwa hiyo inashauriwa kupulizia kiuadudu kwa kubadili ili
kuepuka usugu wa viuatilifu. Mdudu huyu ana hatua nne za ukuaji amabazo ni; Yai,
funza/kiwavi, bundo/pupa na kipepeo. Hatua ambayo ni mbaya sana ni ya funza/kiwavi kwani
funza ndio huaribu mimea.

Viuadudu ambavyo hudhibiti wadudu hawa ni;
โžข Cutter 112 EC (Acetamiprid 64 g/l + Emamectin Benzoate 48 g/l): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Crotale 46 EC (Indoxacarb 30 g/โ„“ + Acetamiprid 16 g/โ„“): Kipimo: 1โ„“/ha au 20 โ€“ 40 mโ„“
โžข Triumph 692 EC (Profenofos 600 g/โ„“ + Lambdacyhalothrin 60 g/โ„“ + Acetamiprid 32 g/โ„“): Kipimo: 250 mโ„“/ha au 20 mโ„“ / 20 โ„“.
โžข Evisect 50 SP (Thiocyclam 50 %): Kipimo: 500 โ€“ 750 g/ha (or 25 g / 20 L. Hii ndio kiuadudu bingwa No.1 kwa hawa wadudu, unapopulizia hakikisha kila jani linashika kiuadudu na rudia kupulizia kila baada ya siku 7 โ€“ 14 kama wadudu bado wapo, kagua mimea yako kabla ya kupulizia.
โžข Uniron 100 EC (Novaluron 100 g/โ„“): Kipimo: 350 mโ„“/ha (au 20 mโ„“ / 20L
NB: Chagua viuadudu 3 na pulizia kwa kubadili.

MAGONJWA
Bakajani wahi (Early Blight)
Ni ugonjwa wa fangasi ukungu unaoshambulia mimea ya nyanya kwa kiasi kikubwa. Ugonjwa huu hushambulia zaidi katika kipindi cha mvua . Dalili za ugonjwa huu ni kuwa na madoa madogo madogo yenye rangi nyeusi au rangi ya kahawia kwenye majani hasa ya chini, matunda na shina. Miche midogo kwenye kitalu inaposhambuliwa hunyauka na kufa, na miche mikubwa hudondosha majani na matunda na kunyauka kwa shina na hatimaye kufa.

Mashambulizi ya bakajani wahi (Early blight)

Udhibiti
Hakikisha usafi wa shamba na ngโ€™oa masalia ya mazao na kuchoma moto mara moja baada ya kuvuna.Zingatia kilimo cha mzunguko wa mazao. Tumia viuatilifu sahihi kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

Baadhi ya viuakuvu venye uwezo wa kudhibiti ugonjwa huu ni
โžข Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/โ„“ + Tebuconazole 277 g/โ„“): Kipimo: 400 โ€“ 600 mโ„“/ha (au 16 โ€“ 24 mโ„“ /20 L
โžข Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 – 2.00 kg/ha (au 60 to 80 g /20
โžข Banko 720 SC (Chlorothalonil 720 g/โ„“): Kipimo: 1.4 – 2.1 โ„“ /ha (au 50 – 80 mโ„“ / 20 L
โžข Banko 500 SC (Chlorothalonil 500 g/โ„“): Kipimo: 2 – 3 โ„“ /ha (au 60 – 100 mโ„“ / 20 L
โžข Cuprocaffaro 50 WP (Copper oxychlorid 500 g/kg): Kipimo: 2.7 – 3 kg /ha (au 50 – 100 mโ„“ / 20 L

Bakajani chelewa (Late blight)

Ni ugonjwa hatari sana hasa katika kipindi cha mvua na baridi ya wastani. Dalili za ugonjwa huu ni kuwa na mabaka makubwa yenye majimaji kwenye matunda, shina na hata majani. Mabaka yenye majimaji hutokea hasa sehemu ya juu ya matunda. Mimea inaposhambuliwa na ugonjwa huu hufa katika kipindi kifupi.

Madhara ya bakajani chelewa ( late blight)

Udhibiti
Zingatia kilimo cha mzunguko wa mazao. Zingatia kanuni za kilimo bora kama kupogolea majani, kusega na kutumia matandazo. Ondoa masalia ya mazao shambani mara moja baada ya mavuno kupunguza vimelea shambani. Tumia viuatilifu sahihi kwa kufuata maelekezo ya wataalum.
Baadhi ya viuakuvu venye uwezo wa kudhibiti ugonjwa huu ni
โžข Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/โ„“ + Tebuconazole 277 g/โ„“): Kipimo: 400 โ€“ 600 mโ„“/ha (au 16 โ€“ 24 mโ„“ /20 L
โžข Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 – 2.00 kg/ha (au 60 to 80 g /20
โžข Banko 720 SC (Chlorothalonil 720 g/โ„“): Kipimo: 1.4 – 2.1 โ„“ /ha (au 50 – 80 mโ„“ / 20 L
โžข Banko 500 SC (Chlorothalonil 500 g/โ„“): Kipimo: 2 – 3 โ„“ /ha (au 60 – 100 mโ„“ / 20 L
โžข Cuprocaffaro 50 WP (Copper oxychlorid 500 g/kg): Kipimo: 2.7 – 3 kg /ha (au 50 – 100 mโ„“ / 20 L
โžข Ivory 72W.

Madoadoa na mnyauko bacteria.
Mnyauko bacteria ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria jamii ya Pseudomonas solanacearum ambao husababisha mnyauko na kufa kwa mimea ghafla. Dalili za maambukizi ya ugonjwa huu huonekana mara tu matunda yanapoanza. Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu huishi ardhini katika udongo kwa muda mrefu na hushambulia mimea kupitia mizizi, au majeraha katika mimea wakati wa kuhamisha miche toka kitaluni na kupandikiza. Mazingira bora kwa bakteria hawa kufanya mashambulizi ni hali ya joto na unyevunyevu katika udongo.

Vimelea hawa wakishaingia katika mishipa ya mimea huziba njia za mfumo wa mzunguko wa
maji katika mimea hivyo mimea hunyauka kwa haraka, bali rangi ya mimea hubakia na rangi
ya kijani na bila madoa. Dalili hii husaidia kutofautisha ugonjwa huu na ule wa mnyauko fusari.
Dalili nyingine zinazotofautisha huu na mnyauko fusari ni pale unapokata shina katika sehemu
ya chini karibu na udongo, sehemu ya katikati ya ndani huwa na majimaji yenye rangi ya
kahawia na hatimaye kuwa na tundu. Namna nyingine ya kutofautisha mnyauko bakteria na
mnyauko fusari pamoja na mnyauko vetisilia ni kukata shina na kutumbukiza katika glasi ya
maji. Endapo majimaji ya rangi ya maziwa yatatoka, ni udhibitisho wa kuwa ugonjwa husika
ni mnyauko bakteria. Namna nyingine ya kutofautisha magonjwa haya ni kuwa, katika
mnyauko bakteria, mimea huanza kunyauka kutokea juu wakati mnyauko fusari na mnyauko
vetsilia mimea huanza kunyauka chini kwenda juu.

Mnyauko bacteria

Madoadoa yanayosababishwa na bacteria

Udhibiti
Tumia aina ya nyanya zinazohimili na kustahimili mashambulizi, tumia mzunguko wa mazao wa muda mrefu, hasa kwa kuhusisha mazao jamii ya mtama, usipande nyanya katika shamba lililopandwa migomba msimu uliotangulia. Zamisha maji shambani. Hakuna viuatilifu vinavyofanya vizuri lakini dawa yoyote yenye copper inasaidia kupunguza tatizo hili,

Baadhi ya viuakuvu venye uwezo wa kudhibiti ugonjwa huu ni
โžข Cuprocaffaro 50 WP (Copper oxychlorid 500 g/kg): Kipimo: 2.7 – 3 kg /ha (au 50 – 100 mโ„“ / 20 L

Mnyauko Fusari ( Fusarium wilt)
Ni ugonjwa hatarii wa ukungu/fangasi jamii ya Fusarium oxysporum. Dalili za ugonjwa huu ni kudumaa, kubadilika rangi na kuwa njano na kahawia na kisha kunyauka. Vimelea wa ugonjwa huu huishi ardhini na hushambulia miea kupitia katika mizizi. Vimelea wakishaingia huziba mishipa ya kupandisha maji (xylem) na hivyo miea husinya na kushindwa kuzaa na hatimaye kufa.


Waweza kutambua ugonjwa huu kwa kuchubua shina katika sehemu ya karibu na ardhi kwenda juu na utaona rangi ya shina ikiwa imebadilika na kuwa ya kahawia, sehemu ya juu karibu na ganda. Tofauti na mnyauko baktria ambapo sehemu ya katikati ndio hubadilika rangi na ile ya nje karibu na ganda huwa nyeupe. Mashambulizi ya mnyauko fusari huenda kwa kasi ikilinganishwa na yale ya mnyauko vetisilia na hiyo diyo tofauti kubwa ya magonjwa haya.


Ugonjwa huu hushamiri zaidi katika mazingira ya joto na udongo wenye tindikali kiasi. Ni rahisi kuchanganya kati ya ugonjwa huu na ule wa mnyauko vetisilia kwani hufanana sana. Vimelea wa ugonjwa huu hushamiri sana katika mazingira ya joto na sehemu yenye udongo wenye majimaji.

Hakuna kiuatilifu aina yoyote kinachoweza kutibu ugonjwa huu kwa 100% hivyo inashauriwa mara baada ya ugonjwa kujitokeza, ngโ€™oa na choma moto mimea yote iliyoathirika na baada ya hapo pulizia dawa za ukungu mimea iliyobaki.


Njia nyingine za kudhibiti ni kutumia mzunguko wa mazao kwa kupanda nyanya katika shamba husika mara moja kila baada ya miaka minne. Katika kipindi hicho pia epuka kupanda mazao jamii ya nyanya kama vile ngogwe, pilipili, biringanya, n.k


Ni muhimu pia kudhibiti minyoo fundo kwani hii hudhoofisha mimea na kusababisha vidonda na hivyo kurahisisha kujipenyeza kwa vimelea wa mnyauko fusari.

Viuatilifu hivi hapa chini huweza kupunguza tatizo kwa asilimia furani.
โžข Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/โ„“ + Tebuconazole 277 g/โ„“): Kipimo: 400 โ€“ 600 mโ„“/ha (au 16 โ€“ 24 mโ„“ /20 L
โžข Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 – 2.00

Ungonjwa wa kata kiuno.

Ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya ukungu (fungi) vilivyo tapakaa katika udongo sehemu nyingi. Kuwepo kwa msongamano wa mimea na kukosekana kwa mtiririko bora wa maji ardhini husababisha mazingira bora ya kuenea kwa mashambulizi ya ugonjwa huu. Ugonjwa huu hushambulia zaidi miche vitaluni na dalili zake ni kunyauka ghafla kwa miche sentimita chache usawa wa ardhi. Maji yakizidi ugonjwa huu huathiri zaidi.

Kata kiuno ( Damping off)
Udhibiti.

Tumia mbegu ambazo zina chanjo ya mbegu na ni vyema kabla ya kusia hata kam mbegu ina dawa ni vizuri kuweka dawa tena. Chanjo nzuri ya mbegu ni Seed plus 30 WS (Imidacloprid 100g/Kg + Metalaxyl 5g/Kg + Carbendazim 5g/kg). kipimo ni 10g za dawa unaweka kwenye kilo 4 za mbegu lakini kwa mbegu za mbogamboga unafanya kukadiria tu, haina madhara hata dawa ikizidi.

Pia mara tu baada ya miche kuota tumia dawa ya ukungu kama vile:
โžข Ivory M 72 WP (Mancozeb 64 % + Metalaxyl 8 %): Kipimo: 50g/20L
โžข Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/โ„“ + Tebuconazole 277 g/โ„“): Kipimo: 400 โ€“ 600 mโ„“/ha (au 16 โ€“ 24 mโ„“ /20 L
โžข Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 – 2.00

Ubwiri unga.
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu, dalili zake kwenye majiani utaona ungaunga ua rangi kama majivu.

Ubwiri unga ( Powdery mildew)

Udhibiti.
โžข Eminent Star 312.5 SE (Chlorothalonil 250 g/โ„“ + Tetraconazole 62.5 g/โ„“) Kipimo: 2 โ„“/ha (au 80 mโ„“20 L
โžข Procure 480 SC (Triflumizole 480 g/โ„“): Kipimo: 500 โ€“ 1000 mโ„“ /ha (au 20 – 40 mโ„“ / 20 L
โžข Evito T 477 SC (Fluoxastrobin 200 g/โ„“ + Tebuconazole 277 g/โ„“): Kipimo: 400 โ€“ 600 mโ„“/ha (au 16 โ€“ 24 mโ„“ /20 L
โžข Glory 750 WG (Mancozeb 700 g/kg + Azoxystrobin 50 g/kg): Kipimo: 1.50 – 2.00 kg/ha (au 60 to 80 g /20

Magonjwa ya virusi
Magonjwa haya huambukizwa kupitia mbegu ama husambazwa na wadudu kama nzi weupe, wadudu mafuta (Vimamba), wanyama ikiwa ni pamoja na binadamu kwa kupitia vifaa vya kazi. Mashambulizi makali huonekana wakati wa joto kali na ukame. Dalili za magonjwa haya ni kudumaa na majani kukunjamana yakipinda kuelekea juu, kutoa matawi mengi na majani kuwa na rangi ya njano, nyeupe au zambarawe. Moja ya magonjwa ya virusi ni Tomato Mosaic Virus ( TMV)

Tomato Mosaic Virus ( TMV)-Ugonjwa wa virusi kwenye nyanya.

Udhibiti
Ondoa mara moja mimea iliyo shambuliwa na kuiharibu ( choma moto) mbali na shamba, zingatia usafi wa shamba, thibiti wadudu waenezao virusi na kusafisha vifaa vya kupogolea kama visu kila unapomaliza kuhudumia mmea mmoja. Epuka kuvuta sigara kwenye shamba la nyanya na dhibiti wadudu hasa nzie weupe.

Matatizo mengine.
Matunda kupasuka

Matunda huweza kupasuka yanapokuwa makubwa karibia na muda wa kukomaa. Ipo mipasuko ya mviringo na mingine yenye sura ya nyota. Mipasuko hii hutokea kutokana na kutokuwa na umwagiliaji wenye mpangilio mzuri, mara maji mengi mara kidogo. Hali hii hujitokeza zaidi wakati wa vipindi vya jua kali na mvua vinapofuatana. Tatizo hili husababisha hasara kwa mkulima kwani matunda hupoteza thamani na pia majeraha husababisha kuoza na hivyo kupunguza thamani na hatimaye mauzo kidogo

Kupasuka kwa matunda
Udhibiti.

Kuwa na mpangilio mzuri wa umwagiliaji. Matumizi ya umwagiliaji kwa mjia ya matone huepusha tatizo hili na pia weka mbolea kama inavyoshauriwa hasa zenye calcium.
Mwisho


Muongozo huu, wa kilimo cha nyanya, umeandaliwa na Agronomist Peter (0744529070) kutoka kampuni ya UPL Tanzania na Ayegro Group Ltd na baadhi ya taarifa zimenukuliwa kutoka vyanzo tofauti tofauti vya Tanzania Horticulture Association (TAHA)
Kilimo ni sayansi

leave your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Ads
Tsh. 1,800 (Negotiable)
Tsh. 1,500 (Negotiable)
Tsh. 1,000 (Negotiable)
Tsh. 30,000 (Negotiable)
Featured Ads
Top
Translate ยป